ExploreTrendingAnalytics
Nostr Archives
ExploreTrendingAnalytics
BITCOINSAFARITZ45d ago
Kwaheri Jerome Powell, karibu Kevin Warsh. Rais wa Marekani, Donald Trump, leo ametangaza rasmi uteuzi wa Kevin Warsh kuwa Mwenyekiti mpya wa Federal Reserve (FED), hatua inayozua mjadala mkubwa hasa katika masoko ya fedha na ulimwengu wa teknolojia ya kifedha. Katika hotuba na maelezo yake ya awali, Kevin Warsh ameonesha mtazamo wa kipekee kuhusu Bitcoin na teknolojia ya blockchain kwa ujumla. Warsh ameeleza kuwa anaiona Bitcoin kama rasilimali muhimu inayoweza kusaidia watunga sera kuelewa kama sera zao za kifedha zinafanya kazi ipasavyo au la. Kwa maneno yake, Bitcoin inaweza kuwa kama “polisi mzuri wa sera” kwa sababu huonesha wazi athari za maamuzi ya kifedha, hasa pale ambapo sera mbaya husababisha kuporomoka kwa imani ya fedha za kawaida. Zaidi ya hilo, Warsh amesisitiza kuwa Bitcoin siyo tu chombo cha kifedha, bali pia ni programu mpya na ya kisasa zaidi (the newest and coolest software) inayofungua milango ya mambo ambayo awali hayakuwezekana. Kwa mtazamo wake, teknolojia hii ina uwezo wa kubadilisha mifumo ya kifedha, kuongeza uwazi, na kutoa mbadala kwa mifumo ya jadi inayodhibitiwa sana na benki kuu. Kauli hizi zinaashiria mwelekeo mpya ndani ya FED, ambapo teknolojia za kidijitali kama Bitcoin zinaweza kuangaliwa sio kama tishio, bali kama kielelezo na chombo cha kujifunza kwa watunga sera za uchumi. Hii ni habari kubwa kwa jumuiya ya Bitcoin na crypto duniani. 🚀
💬 0 replies

Replies (0)

No replies yet.