Huko Afrika Kusini, leo kuna mkutano mkubwa sana unaoendelea uitwao Adopting Bitcoin Cape Town, ambao umeanza leo Day 01 na utaendelea kesho Day 02, ikiwa ni siku ya mwisho ya mkutano huo muhimu kwa mustakabali wa Bitcoin barani Afrika.
Lengo kuu la mkutano huu ni kuwakutanisha watu kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, pamoja na miradi tofauti ya Bitcoin inayofanyika barani Afrika, ili kujadili kwa kina masuala yanayohusiana na teknolojia ya Bitcoin. Washiriki wanajadili namna bora ya kufikisha elimu sahihi ya Bitcoin kwa Waafrika, kuvunja dhana potofu, na kuhakikisha jamii inaelewa Bitcoin kama teknolojia ya kifedha huru, siyo skamu wala kamari.
Mjadala mkubwa pia unaangazia jinsi ya kujenga Bitcoin circular economy barani Afrika, yaani mfumo ambapo watu wanapata kipato kwa Bitcoin, wanaitumia kulipia bidhaa na huduma, bila kulazimika kubadilisha mara kwa mara kwenda kwenye fedha za kawaida. Hili ni jambo muhimu sana kwa Afrika, hasa kwa nchi zinazoathiriwa na mfumuko wa bei, ukosefu wa ajira, na changamoto za mifumo ya kifedha ya jadi.
Zaidi ya hayo, mkutano huu unatoa fursa mbalimbali katika industry ya Bitcoin, ikiwemo ajira, ujasiriamali, maendeleo ya teknolojia, elimu ya kifedha, pamoja na nafasi za kushiriki kwenye miradi ya kimataifa ya open-source. Watoa mada ni watu wenye uzoefu mkubwa, wanaotoa βmadiniβ ya maarifa ambayo siyo poaah aiseee π₯βni elimu ya vitendo kabisa.
Uzuri wa mkutano huu ni kwamba unafanyika pia kwa livestream kupitia YouTube, hivyo hata kama haupo Cape Town unaweza kujifunza moja kwa moja. Kesho ni Day 02 na siku ya mwisho, bado hujachelewa kama uko serious na unataka kuelewa Bitcoin kwa undani.
π YouTube channel ya Adopting Bitcoin Cape Town:
https://www.youtube.com/live/SywqlHeAUDI?si=08xMGYNzZdYIFbAz
Ni muhimu sisi kama Watanzania, hasa vijana, tuamke, tujifunze kutoka kwa wenzetu wa Afrika wanaofanya makubwa kwenye teknolojia hii. Bitcoin ni future, na elimu ndiyo ufunguo. π